Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama aachwa tena Zambia

8ea77d69df689d2564dfbf1d32c46d70 Chama aachwa tena Zambia

Tue, 10 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

NYOTA wa Simba, Clatous Chama hayumo katika kikosi cha timu ya taifa ya Zambia (The Chipolopolo Stars) kilichotangazwa na Kocha Mkuu Milutin “Micho” Sredejovic.

Micho juzi alitangaza kikosi cha awali cha majina 26 kwa ajili ya mchezo wa Kundi H wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2021, dhidi ya Botswana.

Kikosi hicho kina makipa wanne, mabeki sita, viungo watano na washambuliaji 11.

Hivi karibuni Micho alimuacha Chama pamoja na Larry Bwalya wote wa Simba katika kikosi cha Chipolopolo ambacho kilipoteza dhidi ya Kenya Oktoba 9,2020 kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki.

Chama na Bwalya walishindwa kufika kwa wakati katika kambi hiyo baada ya kuchelewa ndege kutoka jijini Dar es Salaam ambako walikuwa na klabu yao ya Simba.

Makipa wanaounda kikosi hicho ni Lameck Siame, Allan Chibwe, Sebastian Mwange na Jackson Kakunta.

Wakati Benson Sakala ndiye anayeongoza mabeki wanaounda kikosi hicho cha awali.

Wengine ni Kondwani Chiboni, Zachariah Chilongoshi, Tandi Mwape, Luka Banda na Dominic Chanda.

Enock Mwepu ni miongoni mwa viungo wakati wengine ni Klings Kangwa, Kelvin Kapumbu, Leonard Mulenga na Chaniza Zulu.

Washambuliaji waliomo katika kikosi hicho ni Kelvin Mubanga, Evans Kangwa, Collins Sikombe, Lubambo Musonda, Emmanuel Chabula, Gamphani Lungu, Amity Shamende, Bruce Musakanya, Fashion Sakala, Augustine Mulenga na Justin Shonga.

Zambia, washindi wa fainali za Afcon 2012 watakuwa wenyeji wa mchezo wa kwanza utakaofanyika Novemba 12 kwenye Uwanja wa Taifa wa Mashujaa jijini hapa.

Mchezo mwingine utashudia Zebra wa Botswana wakiwa wenyeji wa Zambia katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Michezo, Harare Novemba 16.

Algeria kwa sasa wanaongoza Kundi H wakiwa na pointi sita baada ya kushuka dimbani mara mbili.

Zambia hadi sasa haina pointi hata moja kufuatia vichapo vya mabao 5-0 na 2-1 dhidi ya Algeria na Zimbabwe.

Chanzo: habarileo.co.tz