Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama, Wawa, washusha presha Simba

Wawapic Chama, Wawa, washusha presha Simba

Fri, 23 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By THOBIAS SEBASTIANWENYEWE wamerejea, hiyo ndio kauli pekee unayoweza kutoa baada ya kurejea nchini kwa mastaa wa Simba, Clatous Chama na Pascal Wawa, ambao waliikosa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons ugenini jana huko Sumbawanga kwa bao 1-0.

 

Habari za ndani zinasema tayari wawili hao wamesharejea nchini ambapo alianza  Wawa aliyeingia nchini jana Alhamisi huku Chama akitarajiwa kutua usiku wa leo kutoka kwao Zambia na wote mara moja watajiunga na wenzao katika progamu ya mazoezi itakayofanyika Jumamosi.

 

Kukosekana na Chama na baadhi ya nyota wa Simba kumepelekea utetezi kwa mashabiki wengi wa timu hiyo kuwa ndio kulichangia kwa kiasi kikubwa Simba ipoteze mechi ya jana kwa kichapo cha bao 1-0 lililofungwa na Samson Mbangula

 

Chanzo: mwanaspoti.co.tz