Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama: Wanachi vuteni viti, burudani kubwa inakuja

Chama MsjSMJ.jpeg Chama na Pacome

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutambulishwa mara mbili, kiungo mpya wa Yanga, Clatous Chama amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa wavumilivu na kukutana uwanjani, anaenda kupiga kazi kushirikiana na wenzake kufikia malengo ya msimu wa 2024/25 hasa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chama amesema kuwa amerejea nchini kwa mara nyingine na msimu huu atakuwa kwenye timu nyingine na tayari amejiunga rasmi na wachezaji wenzake kwa maandalizi ya michuano iliyopo mbele yao ikiwemo Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kiungo huyo amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza baada ya kutamatika na sasa anaenda kuungana na Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzoua.

“Nashukuru kwa mashabiki wa Yanga wamenipokea na kunikaribisha vizuri, nimeanza rasmi mazoezi na program ya timu kikubwa wananchi tukutane uwanjani,” amesema kiungo huyo na kuwahidi kufanya vizuri ndani ya kikosi cha timu hiyo.

Nyota huyo amejiunga na kikosi cha mabingwa hao kwa msimu wa 2024/25 huku Yanga wametupia dongo kwa watani zao Simba kwa kuweka ujumbe wenye swali kuwa “Kwa Mkapa mtakuja kweli?

Chama ameonekana mwenye furaha akiwa na Pacome kiungo wa kazi ambaye watakuwa pamoja kwa msimu ujao

Klabu hiyo umepanga kumtambulisha kiungo huyo mara tano, wameshamtambulisha mbili na kesho wataendelea na zoezi hilo. Tayari Yanga imetambulisha wachezaji watano akiwemo Chama, Aziz Andamwile, Prince Dube na Khomeini Abubakar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live