Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama: Tunawasubiri kwa hamu Power Dynamos

Chama Na Ngoma Chama: Tunawasubiri kwa hamu Power Dynamos

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clotus Chama amesema wanaisubiri kwa hamu Power Dynamos kutoka nchini kwao Zambia watakayocheza nayo Agosti 6, 2023 ndani ya Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Chama anasema Dynamos ni timu ambayo ilikuwa imara sana miaka ya nyuma na sasa ndio mabingwa wa Zambia hivyo wanategemea kupata ushindani utakaowasaidia wao kujua wapi waongeze zaidi.

"Ile ni timu ambayo mimi mwenyewe nilitamani sana kuichezea miaka ya nyuma, kweli nilifanikiwa kuichezea kwa takriban miezi sita kisha nikaenda ZESCO," alisema.

Chama alisema anawaombea kwenye mechi za Klabu Bingwa wafanye vizuri ili ikiwezekana wakutane ili waweze kuwapiga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live