Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama: Simba tulieni, mambo mazuri yanakuja

Chama Goal Vs JKT Chama: Simba tulieni, mambo mazuri yanakuja

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya Wekundu wa Msimbazi, Simba kuvuna pointi 18 kati ya 21 kwenye michezo saba ya Ligi Kuu Bara ikiwa chini ya Abdelhak Benchikha, kiungo fundi kwenye kikosi hicho, Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka' ameeleza kuwa bado wanaendelea kujifua ili kuwa bora zaidi kama timu.

Chama ambaye ameifanya Simba kuvuna pointi nne kwenye michezo miwili kati ya mitatu iliyopita ya ligi kwa kufunga dhidi ya JKT Tanzania na Azam FC, alisema malengo yao kama timu ni kuchukua ubingwa hivyo wataendelea kuweka mkazo kwenye kila mchezo na kufanyia kazi mapungufu yao ili kufanikisha hilo.

"Tangu tuanze tulikuwa na makosa madogomadogo lakini naona kama  bado tunaendelea kujitafuta, nafasi ya pili sio mbaya nahisi wametupita pointi nne (Yanga) kwa hiyo tutaendelea kupunguza utofauti huo kwa sababu malengo yetu ni kuchukua ubingwa wa ligi," alisema fundi huyo na kuongeza;

"Mashabiki wa Simba wategemee mazuri kutoka kwenye timu, watuombee na kutusapoti na sisi tutaendelea kupambana kwa ajili yao, tunaomba watupe sapoti,"aliongeza staa huyo wa Zambia.

Akiongelea bao ambalo alifunga dhidi ya JKT Tanzania, Chama alisema huwa anapokuwa uwanjani kwake kufunga sio kitu cha ajabu ambacho anakipa kipaumbele na wala huwa hajivunii jambo muhimu kwake huwa ni kuona timu inapata matokeo mazuri kwenye kila mchezo maana unaweza kufunga halafu mkapoteza.

Kwa upande wake, Benchikha anafurahi kuona fundi huyo amekuwa sehemu ya upatikanaji wa matokeo ambayo wameyapata kwenye michezo hiyo migumu ambayo ilifuata,"Tumekuwa na ratiba ngumu lakini jambo muhimu ni kwamba tumepata matokeo chanya, tunaendelea na safari, tunatakiwa kupiga hatua kama timu."

Tangu Chama arejee kikosini akitokea kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika ambazo zilifanyika huko Ivory Coast akiwa na timu yake ya taifa la Zambia, ameinogesha Simba kwenye eneo la mwisho la ushambuliaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live