Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama, Musonda watokea benchi Zambia ikishinda 2-0

FAZ Chama, Musonda watokea benchi Zambia ikishinda 2-0

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Clatous Chama na Kennedy Musonda wametokea benchi kuichezea Zambia dakika za mwishoni ikishinda 2-0 dhidi ya Lesotho kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Katika mchezo huo wa Kundi H uliofanyika Uwanja wa Volkswagen Dobsonville Jijini Johannesburg, Afrika Kusini - mabao ya Chipolopolo yote yamefungwa na mshambuliaji wa Leicester City, Patson Daka dakika ya 14 na 69.

Kiungo wa Simba, alianza kuingia dakika ya 81 kuchukua nafasi ya Kings Kangwa wa Red Star Belgrade ya Serbia, akafuatia mshambuliaji wa Yanga, Musonda kuingia dakika ya 90 kuchukua nafasi ya mfungaji wa mabao, Patson Daka.

Ushindi wa huo unaifanya Zambia ifikishe pointi tisa katika mchezo wa nne na kupanda kileleni ikiizidi Ivory Coast pointi mbili ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live