Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama, Mgunda wang'ara tuzo za TFF

Chama Na Mgunda Chama, Mgunda wang'ara tuzo za TFF

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Simba, Clatous Chama amechaguliwa kuwa mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi kuu ya NBC msimu wa 2022/23.

Chama ananyakua tuzo hiyo akiwagaragza John Bocco (Simba SC) na Fiston Mayele (Yanga)

Kwa mezi Desemba Chama amefunga mabao mawili na kutoa pasi tano za mabao katika michezo mitano aliyocheza.

Kocha wa Simba, Juma Mgunda amechaguliwa kuwa kocha Bora wa mwezi Desemba wa Ligi kuu ya NBC msimu wa 2022/23.

Mgunda ananyakua tuzo hiyo akiwapiku Nasreddine Nabi (Yanga) na Hans Van Pluijm(Singida Big Stars).

Mgunda aliiongoza Simba katika michezo mitano mwezi Desemba akishinda minne na kutoa sare mchezo mmoja.

Aidha Tuzo ya Meneja bora wa Uwanja kwa mwezi Desemba imekwenda kwa Meneja wa Uwanja wa Manungu uliopo Mkoani Morogoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live