Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama, Mayele nani kusepa?

Chama Mayele Pic Chama na Mayele.

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Clatous Chama moja kati ya wachezaji muhimu sana ndani ya Kikosi cha Simba, yeye ndiyo roho ya timu.

Chama ni kipenzi cha Wanamsimbazi, hata hivyo amehusishwa na kutakiwa na Klabu nyingine kwenye kipindi hiki cha usajili na hivyo tetesi hizo kuzua taharuki miongoni mwa mashabiki.

Mayele Fiston ndiye mchezaji pekee mwenye uhakika wa kukupa magoli katika kila mechi atakayocheza ndani ya Young Africans Sports.

Mashabiki wa Yanga huwaambi kitu kuhusu Mayele, hayo sio tu Mapenzi bali ni Mahaba yao kwa Mchezaji huyo wa DRC Congo.

Chama, Mayele wote wana Mkataba wa mwaka mmoja uliyobakia na huwenda hiyo ikawa sababu ya tetesi zote za kuhusishwa na timu nyingine kutaka kusajiliwa.

Mayele anapewa asilimia kubwa zaidi kuondoka Yanga SC msimu huu kuliko Chama ndani ya Simba SC kutokana na Ofa zinazodaiwa kufika mezani ingawaje wote bado wanahitajika ndani ya Klabu zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live