Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama: Kila kombe ni muhimu kwetu

Chama Toyota Msz Clatous Chota Chama.

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Clatous Chama amesema kuwa kila kombe kwao ni muhimu msimu huu, hivyo kama wachezaji wamejiandaa kuwapa burudani mashabiki wao 'Wananchi'.

Chama amesema hayo baada ya Yanga kufanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Toyota Cup kwa kuwabamiza wenyeji Kaizer Chiefs kwa bao 4-0 nchini mwao jana Jumapili, Julai 28, 2024.

“Mchezo ulikuwa mzuri na mgumu lakini baada ya sisi kuanza kufunga mechi imekuwa rahisi kidogo. Hali ya hewa ya hapa ni baridi sana tofauti na Dar es Salaam, lakini ukiingia uwanjani ukianza kukimbia damu inachemka, angalau.

“Kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi, mimi ninawashukuru mashabiki kwa sapoti yao na maombi yao, ninahisi hiyo Mwananchi Day itakuwa siku nzuri, ninawakaribisha tuje kusherehekea pamoja.

“Kwetu sisi kila kikombe ni muhimu na tumeshachukua hiki, sasa itatupa nguvu na morali zaidi sisi kama wachezaji na wao mashabiki watakuwa na furaha, tuombe msimu uwe mzuri,” amesema Chama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: