Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama, Kagere watengewa mamilioni, Platinum kazi wanayo...

Fungu Pic Data Chama, Kagere watengewa mamilioni, Platinum kazi wanayo...

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Waandishi WetuMore by this Author SIKU nne tu kabla ya kuvaana na FC Platinum ya Zimbabwe katika pambano la marudiano la Ligi ya Mabingwa Afrika, Clatous Chama, Luis Miquissone na nyota wengine wa Simba wametengewa mamilioni ya fedha watakayovuna iwapo watawang’oa Wazimbabwe hao.

Simba itakuwa wenyeji wa Platinum katika mechi itakayopigwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, huku wakiwa na kazi ya kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 ugenini, ili kujihakikisha wanatinga hatua ya makundi kwa mara yao ya tatu.

Wekundu hao wa Msimbazi walitinga hatua hiyo ya makundi ya ligi hiyo mara ya kwanza 2003 na 2018-2019, na kwenye mechi yao dhidi ya Wazimbabwe wanahitaji ushindi wa mabao 2-0 ili kupindua meza na kusonga mbele, huku wakibebwa na rekodi zao kwenye uwanja wa nyumbani.

Katika kuhakikisha wanatinga hatua hiyo, mabosi wa Msimbazi wameamua kuwatia mzuka kina Chama kwa kuwaahidi mamilioni ya fedha kama wataing’oa Platinum.

Ipo hivi. Mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kumalizika kwa Simba kushinda mabao 4-0 dhidi ya Ihefu, Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez akiwa sambamba na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Dk Mohammed Janabi waliwavamia nyota wao na benchi la ufundi katika chumba cha kubadilishia nguo na kuteta nao kwa muda mfupi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz