Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama: Hakuna ugomvi wowote ndani ya Simba

Chama Complete Chama: Hakuna ugomvi wowote ndani ya Simba

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Zambia anayechezea Simba SC, Clatous Chama amesema anakiri kwamba hawakucheza vizuri kwenye michezo mitatu iliyopita lakini si kwamba kuna ugomvi ndani ya timu.

Chama amesema, kwa sasa Simba hawatakiwi kunyosheana vidole na badala yake waungane, waisapoti timu ili waweze kurudi kwenye matokeo yao ya kuwapa furaha Wana-Simba.

"Msimu uliopita Champion League tulianza vibaya, tulipoteza dhidi ya Horoya, tukaja tukapoteza dhidi ya Raja lakini baadaye tuliamka na kupata matokeo yaliyotuwezesha kuvuka kwenda hatua iliyofata ya Robo Fainali," alisema Chama.

Simba wamekuwa na wakati mbaya baada ya kupoteza michezo mitatu iliyopita kwa mmoja kufungwa na Yanga, miwili sare dhidi ya Namungo FC (1-1) na dhidi ya ASCE Mimosas (1-1).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live