Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama, Dube wamkosha Gamondi

Gamondi Chama Dube Chama, Dube wamkosha Gamondi

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa mpaka sasa ni wachezaji wapya watano waliosajiliwa kwenye kikosi chake kuelekea msimu ujao wa 2024-2025, Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi ameonekana kufurahishwa na hilo.

Gamondi katika kufurahishwa kwake amebainisha kwamba ujio wa wachezaji hao utaongeza kitu ndani ya kikosi kutokana na kuzingatia mahitaji yake.

“Tumeleta wachezaji wachache watakaoongeza kitu kwenye timu, hatujaleta idadi kubwa ya wachezaji bali wachezaji bora na ni mahsusi kwenye maeneo tulikuwa tuna uhitaji.

“Nina matumaini makubwa na hawa wageni, ila pia tuwape muda wa kuzoea mazingira ya hapa Yanga na pia kuelewa mbinu zetu,” alisema Gamondi.

Wachezaji wapya mpaka sasa waliotambulishwa ndani ya kikosi cha Young Africans kuelekea msimu ujao ni Kiungo mshambuliaji Clatous Chama, mshambuliaji Prince Dube, beki wa kushoto Chadrack Boka, kipa Khumeiny Aboubakar na kiungo mkabaji Aziz Andambwile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: