Stephane Aziz KI wa Yanga na Clatous Chama wa Simba wameendelea kuteuliwa katika vikosi vya timu zao za taifa, Burkina Faso na Zambia.
Baada ya kuwemo katika vikosi vya timu hizo mwezi uliopita kwenye mechi za kirafiki, nyota hao wameitwa katika vikosi vitakavyocheza mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 kwa nchi zao.
Kocha wa Burkina Faso, Hubert Velud amemuita Aziz Ki katika kikosi cha wachezaji 25 kitakachocheza mechi mbili za kuwania kufuzu Kombe la Dunia za kundi A dhidi ya Guinea Bissau nyumbani, Novemba 17 na ugenini dhidi ya Ethiopia, Novemba 21.
Kikosi hicho cha wachezaji 25 wa Burkina Faso kinaundwa na Herve Koffi, Kilian Nikiema, Hilel Konate, Steeve Yago, Issa Kabore, Issoufou Dayo, Adamo Nagalo, Edmond Tapsoba, Fjiga Nasser, Abdoul Razack Guiebre na Valentin Nouma.
Wengine ni Dramane Salou, Blati Toure, Ismahila Ouedraogo, Adama Guira, Trova Boni, Gustavo SangareĀ Cedric Badolo, Sacha Banse, Bertrand Traore, Hassan Bande, Stephane Aziz Ki, Mohamed Konate na Dango Ouattara.
Kwa upande wa Chama naye ameitwa katika kikosi cha wachezaji 25 wa Zambia kitakachocheza nyumbani dhidi ya Congo, Novemba 17 na kisha ugenini dhidi ya Niger, Novemba 21, mechi zote zikiwa za kundi E.
Kocha Avram Grant amewaita makipa Charles Kalumba, Lawrence Mulenga na Francis Mwansa mabeki wakiwa ni Benedict Chepeshi, Stopila Sunzu, Killian Kanguluma, Dominic Chanda, Luka Banda, Roderick Kabwe na Zepheniah Phiri.
Viungo ni Kings Kangwa, Chama, Benson Sakala, Andrew Mupande, Emmanuel Banda, Golden Mafwenta, Rally Bwalya, Lubambo Musonda, Edward Chilufya na Kelvin Kampamba.
Washambuliaji ni Lameck Banda, Patson Daka, Brian Mwila, Fashion Sakala na Evans Kangwa