Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama Aliamsha Moro Kabla ya Mechi

Chama Clat Chama Aliamsha Moro Kabla ya Mechi

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KIUNGO wa Simba, Clatous Chama ameanza kuwapa raha mashabiki wake mapema baada ya kupiga pasi zinazofika eneo husika.

Kocha wa Simba, Pablo Franco aliwapanga Chama, Rally Bwalya na Bernard Morrison kupiga mashuti nje ya 18, pia kupika kona.

Chama alifikisha mashuti yake eneo linalotakiwa, jambo ambalo liliwapa raha mastaa wenzake.

Pablo ni kama anamkabidhi majukumu Chama ya kupiga faulo, kwani amewatenga pembezoni mwa uwanja kupiga faulo, akiwa na Bwalya.

Kwa namna kocha anavyompa majukumu Chama ni dhahiri atampanga mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar, ambao utapigwa Manungu.

Chama alipiga shuti kwa Hassan Dilunga ambaye alitokea katikakati la kundi la wachezaji wengine, huku Meddie Kagere,Chris Mugalu na Sakho wakikimbia kufunga.

Amewatenga mabeki Joash Onyango,Juma Kennedy na Inonga kuwawahi kina Kagere mbele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live