Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadrack Boka ameumia nyonga, apelekwa kufanyiwa vipimo vikubwa

Chadrack Boka.jpeg Chadrack Boka.

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka katika kambi ya timu ya Young Africans iliyopo Afrika Kusini inabainisha kwamba beki wa kushoto, Chadrack Boka anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya MRI kufahamu ukubwa wa jeraha lake.

Boka ambaye amejiunga na Yanga hivi karibuni, alipata maumivu katika mchezo wa juzi wa Mpumalanga Cup dhidi ya FC Augsburg uliochezwa Uwanja wa Mbombela uliopo Mji wa Mpumalanga nchini Afrika Kusini na yanga kuchezea kipigo cha bao 2-1.

Akitoa taarifa ya majeraha ya Boka, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans, Ally Kamwe amesema beki huyo ameumia misuli ya nyonga.

“Chadrack Boka amepata maumivu ya misuli ya nyonga (aductor muscle strain), uchunguzi wa awali wa madaktari wetu wanafikiri inaweza kuwa jeraha la kati la msuli wa nyonga (grade 2 adductor muscle injury).

“Anatarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi ikiwemo na MRI ili kuthibitisha ukubwa wa jeraha lake. Tutatoa taarifa zaidi baada ya vipimo kufanyika,” alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live