Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cesc: Huyu Ronaldo ana balaa

Ronaldo Euro 6 Cesc: Huyu Ronaldo ana balaa

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Arsenal na Barcelona, ambaye kwa sasa ni kocha wa Como inayoshiriki Ligi Kuu Italia, Cesc Fabregas amemsifu staa wa Ureno, Cristiano Ronaldo akisema ameendelea kuwa mtamu zaidi licha ya umri kumtupa mkono.

Ronaldo, ambaye anacheza michuano yake ya sita ya Euro akiwa na umri wa miaka 39, alikuwa sehemu ya kikosi cha Ureno kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Czech katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi.

Licha ya kutofunga bao alionyesha kiwango bora alipokuwa na mpira na muda mwingi aliwafanya washambuliaji wengine kuwa huru.

Akizungumza na BBC Sport, Fabregas alisema:"Namna anavyocheza kijumla ni vizuri zaidi pengine hata ilivyokuwa hapo awali, ulikuwa unamwona timu ikicheza vizuri au vibaya muda wote alikuwa anapata nafasi ama kutengeneza kwa ajili ya wengine, ukimwangalia Ronaldo wa sasa pia anaonekana kujiamini zaidi.

Ronaldo amefunga mabao 58 katika mechi 64 akiwa na Al-Nassr tangu ajiunge na matajiri hao wa Saudi Arabia Januari 2023 akitoka Manchester United.

Alitua Ligi Kuu ya Saudi Arabia baada ya kugombana na kocha wake Erik ten Hag na alifunga mabao 27 katika mechi 54 za michuano yote akiwa na kikosi hicho.

Kwenye kikosi cha Ureno amecheza mechi 208 na kufunga mabao 130.

Chanzo: Mwanaspoti