Waswahili wana msemo usemao"Ng'ombe hachoshwi na pembe zake" ndivyo ilivyo kwa mama mzazi wa Casemiro ambae licha ya ugumu wa maisha alioupitia hkuwahi kuchoshwa na malezi ya kijana wake Casemiro.
Leo Hii Mama wa Casemiro anafaidi matunda ya kile alichokikuza na mara kadhaa Casemiro amekuwa akidhihirisha upendo wake kwa mzazi wake ;
"Mama yangu alikuwa akifanya kazi za majumbani kila siku ya wiki kuanzia Jumapili hadi Jumapili baada ya baba yangu kutuacha nikiwa na umri wa miaka mitatu.
Simkumbuki kabisa Baba yangu na wala sipendi kumjua.Ninachokumbuka vizuri na kujivunia ni kwamba nilipopokea pesa yangu ya Usajili Kwa mara ya kwanza katika soka langu la kulipwa, nilienda moja kwa moja kumnunulia nyumba mama yangu ambaye aliteseka sana na kuhangaika na mimi hadi kufika hapa nilipo sasa."
Casemiro kwa sasa anakipiga katika klabu ya Manchester United ya England baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa katika kikosi cha Real Madrid.