Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Casemiro katika njia za Roy Keane

 Medium (600 X 360) Casemiro afananishwa na Roy Keane

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Teddy Sheringham amemfananisha Casemiro na mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United Roy Keane, akidai Mbrazil huyo ndiye jenerali wa kiungo ambaye klabu hiyo ilikuwa imemkosa kwa muda mrefu na sasa wamempata.

Casemiro amekuwa akisifiwa tangu uhamisho wake wa paundi milioni 70 kutoka Real Madrid kwenda United msimu wa joto, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akiwa na mchango mkubwa katika kuimarika kwa Mashetani Wekundu msimu huu chini ya meneja Erik ten Hag.

Manchester United italazimika kuvumilia kidogo kucheza bila Casemiro kwenye mechi tatu zijazo za Premier League, baada ya Mbrazil huyo kuonyeshwa kadi nyekundu ya kwanza katika maisha yake ya soka akiwa na United, dhidi ya Crystal Palace Jumamosi.

Sheringham alisema kiungo huyo anaweza kufananishwa na Keane, ambaye alionesha viwango vyake kama nahodha wa Manchester United wakati wa misimu minne ya mchezaji huyo Old Trafford. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kubashiri.

Sheringham alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu ya Uingereza katika timu ya United inayoongozwa na Keane, ikiwa ni pamoja na kucheza nafasi muhimu katika msimu wao wa mara tatu mwaka 1998-99.

“Nitasema tu kuhusu Casemiro nadhani ni kama Roy Keane ambaye wamemkosa kwa miaka minane iliyopita,” alisema Sheringham, ambaye alifunga mabao 46 katika mechi 153 za United.

“Jenerali huyo wa kiungo ambaye ana hamu na uelewa wa mchezo wa lini afanye nini ili kuhakikisha kuwa timu yake inafanya vizuri kadri ya uwezo wao.

“Hana wasiwasi tu juu yake mwenyewe, ninampenda.

“Labda alifikiri alipaswa kutekeleza jambo fulani wakati huo (wa kadi yake nyekundu)”

Casemiro hatakuwepo kwenye mechi mbili zijazo za United dhidi ya Leeds kwenye Premier League, pamoja na mechi dhidi ya Leicester. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!.

Kiungo huyo mwenye ushawishi mkubwa atapatikana kwa fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Newcastle. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa na zawadi ya ukaribisho ukijiunga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live