Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Casemiro? Ndo basi tena!

Casemiro Amerejea Casemiro

Tue, 2 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mtangazaji wa televisheni ya beIN Sports, Andy Grey ameangalia uwezekano wa kiungo wa Manchester United kuendelea kuwepo kwenye timu hiyo na kudai, ni ngumu.

Grey amesema maisha ya nyota huyo wa zamani wa Real Madrid yatafika tamati baada ya ujio wa bosi mpya wa klabu hiyo, Sir Jim Ratcliffe na kushuka kwake kiwango kunatia mashaka kama ataendelea kuwepo Old Trafford msimu ujao.

Inaelezwa Man United iko tayari kuachana na Mbrazili huyo ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, ingawa huenda akarejea mwezi huu akiwa fiti.

Kuhusu nafasi ya Casemiro uwanjani, Grey alisema, "Hapana, itakuwa mwisho wake pale (Man United)."

Man United ilimsajili Casemiro kwa Pauni 60 milioni kutoka Real Madrid kwa mkataba wa miaka minne na alifurahia msimu wake wa kwanza akifunga pia bao kwenye fainali ya Carabao Cup na kuipa timu hiyo taji la kwanza baada ya miaka sita.

Baada ya taarifa ya bosi mpya kukata baadhi ya majina kwenye usajili ujao wa wachezaji, mashabiki wa klabu hiyo wamepata hofu juu ya mustakabali wa Casemiro.

Casemiro huenda akacheza mechi ya Kombe la FA dhidi ya Blackburn, huku kocha Erik ten Hag akiwa na matumaini atarudi akiwa fiti kwa ajili ya kuisaidia timu sehemu ya kiungo.

Wakati huo huo, kiungo huyo amehusishwa na klabu kutoka Saudi Arabia, hata hivyo haijafahamika endapo kuna ofa nyingine zitajitokeza kwa ajili yake.

Chanzo: Mwanaspoti