Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Carragher alia na UEFA kufuta goli la ugenini

CARRA Kylian Mbappe akiwa anafunga goli dhidi ya Real Madrid)

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Gwiji wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher amesema kitendo cha Shirikisho la soka barani ulaya UEFA kufuta mfumo wa faida ya goli la ugenini, kumefanya baadhi ya timu zijilinde zaidi kuliko kushambuliwa zikiwa ugenini.

Carragher amesema, Real Madrid walicheza kwa kuzuia muda mwingi kwenye mchezo huo kwa lengo la kupata sare kwasababu walilenga kuzuia tu wasifungwe kwakuwa goli la ugenini halina faida kama ilivyokua awali.

Licha ya kucheza kwa kuzuia muda mrefu, lakini Real Madrid wamepoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0 sekunde kadhaa kabla mchezo haujamalizika na nyota wa timu hiyo, Kylian Mbappe.

Gwiji huyo ambaye kwasasa ni mchambuzi wa Sky Sports, amesema UEFA wafikirie kitu kingine cha kufanya ili timu zicheze mchezo wa kushambulia wakiwa ugenini ili kurudisha ladha ya soka ambayo pengine huenda ikapungua.

Kwa upande mwingine,

Nyota wa PSG Lionel Messi alikosa mkwaju wa penalti katika mchezo huo iliyopanguliwa na kipa wa Madrid, Thibaut Courtois na Messi kuweka rekodi ya kukosa penalty 5 nyingi zaidi kwenye historia ya UEFA sawa na Thierry Henry.

Muda ambao Messi alikoa penalti ndiyo muda ambao Cristiano Ronaldo alikuwa anafunga bao lake la kwanza ndani ya mwaka 2022 katika ukame wa michezo 6 na kuisaidia Manchester United kushinda 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion.

Chanzo: eatv.tv