Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Carragher aipa ushindi Arsenal dhidi ya Man City leo

Jamie Carragher Vs City.jpeg Carragher aipa ushindi Arsenal dhidi ya Man City leo

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gwiji wa zamani wa Klabu ya Liverpool, Jamie Carragher ameipa Klabu ya Arsenal ushindi dhidi ya Man City mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Emirates leo.

Akizungumza Carragher anasema;

"Ninaipa Arsenal, Nadhani Arsenal wanaweza kufanya hivyo kwa faida ya kuwa wanacheza nyumbani na Rodri hachezi, ambaye ni mchezaji mkubwa wa Manchester City, Kwa hivyo ninaipa Arsenal kushinda hii mechi"

"Hiyo itatupa kinyang'anyiro cha ubingwa kati ya sasa na mwisho wa msimu kwa sababu hatuwezi kumudu, kama watu wasioegemea upande wowote, nadhani tunataka mbio za ubingwa ziende mradi tu zinaweza kwenda"

"Msimu uliopita ilifanya hivyo, ilikuwa nzuri kati ya Arsenal na Manchester City lakini hatutaki City wawe mbele hadi kufikia Krismasi na Mwaka Mpya kiasi kwamba timu zingine zipoteze imani"

"Sio nzuri kwa ligi. Natumai Arsenal wanaweza kupata pointi tatu.” amesema Carragher kupitia Metro

Chanzo: www.tanzaniaweb.live