Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Carragher: Unai Emery ndie Kocha Bora EPL

Skysports Carragher Emery 6358597 Carragher: Unai Emery ndie Kocha Bora EPL

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jamie Carragher amemtaja bosi wa Aston Villa, Unai Emery kuwa ndiye Kocha Bora wa Ligi Kuu England msimu huu na kuwatosa makocha mashuhuri kama Jurgen Klopp na Pep Guardiola.

Kocha huyo wa zamani wa Arsenal, Emery alijiunga na Aston Villa akitokea Villarreal, Oktoba 2022 ambapo timu hiyo ilikuwa nje kidogo tu ya timu zinazopambana kushuka daraja. Kocha huyo Mhispaniola amefanikiwa kuifanya timu hiyo kufanya vizuri, ikimaliza nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na kukamatia tiketi ya michuano ya Ulaya.

Na ameendelea kuwasha moto msimu huu, ambapo kikosi hicho kilifika nusu fainali ya Europa Conference League na kuna uwezekano wa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kutokana na kushika nafasi ya nne kwenye ligi.

Katika kipindi chake alichokuwa Villa Park, Emery ameshinda asilimia 57 ya mechi zake kwenye Ligi Kuu England. Hiyo ikiwa rekodi bora kabisa kwenye historia ya timu hiyo kwenye ligi hiyo baada ya makocha waliomtangulia na kuonekana walifanya vizuri, wenyewe walishinda John Gregory (asilimia 41) na Martin O’Neil (asilimia 44).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live