Usajili wa msimu wa kiangazi Erling Haaland ana sifa za kuwa mchezaji bora zaidi kuwahi kumuona kwenye Ligi ya Uingereza, alisema mchambuzi wa michezo Jamie Carragher.
Haaland amecheza akiwa na Manchester City, na kuwa mchezaji wa kwanza EPL kufunga mara tisa katika mechi zake tano za kwanza, huku akifunga mabao matatu mfululizo “Hattrick” dhidi ya Crystal Palace na Nottingham Forest yakiibua matarajio ya hatari kwenye suala ya kinara wa mabao kwenye Epl mwisho wa msimu.
Raia huyo wa Norway aliwasili Uingereza akiwa ni moja ya wachezaji waliotazamwa sana na kutabiriwa makubwa, huku Carragher akiamini kuwa Ligi ya Uingereza inashuhudia kitu maalum kuwa na mchezaji huyo.
Alipoulizwa kutaja klabu gani ilikuwa na dirisha bora na usajili wake wa majira ya joto, Carragher aliiambia Sky Sports News: “Manchester City wamekuwa na dirisha zuri sana. Walipoteza wachezaji wengi wa kushambulia, lakini wamewasajili wachezaji kama (Julian) Alvarez, ambaye tayari anaonekanakuwa bora sana, na Haaland inaonekana ni mchezaji hatari.