Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Carlo Ancelotti aweka ngumu mastaa kutua Real Madrid

Carlo Ancelotti.jpeg Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti

Sun, 6 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti ameweka bayana kua klabu hiyo haina mpango wa kufanya usajili wowote kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Kocha huyo ameeleza hayo kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Rayo Vallecano ugenini, Ancelotti amekua akisistiza jambo hilo mara kadhaa na hii inatokana na klabu hiyo kuhusishwa na wachezaji kadhaa.

Kocha huyo amekua akiamini kikosi cha klabu hiyo kimeimarika na kina wachezaji wa kujitosheleza kabisa na wenye ubora wa hali ya juu, Huku dirisha lililopita klabu hiyo kuongeza mchezaji mmoja tu ili kuboresha kikosi hicho.

Klabu ya Real Madrid imekua ikifanya kazi ya kuongeza mikataba kwa wachezaji wake nyota klabuni hapo kama Karim Benzema, Luca Modric na wengine wakiwa kwenye mazungumzo.

Kocha Ancelotti ambae amefanikiwa kuipatia klabu hiyo taji la 14 la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya huku yeye akifikisha mataji manne na kuweka rekodi kuwa kocha wa kwanza kufanya hivyo, anaamini klabu yake ipo kwenye wakati mzuri na ina wachezaji wazuri hivo haina haja ya kuingia sokoni mwezi Januari kwajili ya kukiinarisha kikosi chao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live