Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Carlo Ancelotti amfagilia Mourinho

Carlo X Mourinho Carlo Ancelotti amfagilia Mourinho

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kuwa Jose Mourinho ni kocha sahihi kabisa wa AS Roma na ulikuwa uamuzi mzuri kwake kuhamia katika klabu hiyo baada ya kuondoka Spurs.

Kocha huyo Mreno mwenye umri wa miaka 59 alichukua mikoba ya Giallorossi mwaka jana na mara moja akapata mafanikio katika kikosi hicho kilichopo mji mkuu wa Italia, kwa kuiongoza klabu hiyo kutwaa taji lao la kwanza kabisa la Uropa Conference.

Roma walichukua viungo muhimu kama Paulo Dybala na Nemanja Matic msimu wa joto, wakitaka kupigania kumaliza nne bora ili waweze kushiriki michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya.

Akiandika katika kitabu cha Ivan Zazzaroni ‘Becoming Mourinho’, Ancelotti alitoa mawazo yake kuhusu Mourinho na uhamisho wa kocha huyo wa Kireno kwenda Roma mwaka jana na Ancelotti akasema kuwa;

“Nimemfahamu José kwa miaka mingi na ninaamini kwamba Roma amembadilisha kocha huyo na Waroma wenyewe. Ni gwiji wa soka, najua hajabadilika, uaminifu wake na akili hazijabadilika.”

Tangu kuwasili kwake mwaka jana, Mourinho amesimamia mechi 73 za Roma kwa jumla, akiwa na wastani wa pointi 1.84 kwa kila mechi. Klabu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Serie A baada ya michezo 12, akijinyakulia pointi 25 baada ya kushinda mechi nane, sare moja na kupoteza michezo mitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live