Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Carlinhos aanza kujifua Yanga

Yanga14511azam Carlinhos aanza kujifua Yanga

Thu, 27 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Waandishi WetuNYOTA mpya wa Yanga SC, Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo 'Carlinhos' ameanza kufanya mazoezi mepesi ya kukimbia katika Uwanja wa Chuo cha Sheria, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Carlinhos alitua nchini Jumanne Agosti 25 akitokea Angola na kuweka rekodi ya kupokewa na mamia ya mashabiki wa timu hiyo ya Wananchi yenye maskani yake Jangwani.

Wakati wenzake wakiendelea na mazoezi ya nguvu chini ya kocha Juma Mwambusi, Carlinhos alikuwa amekaa akiangalia kile ambacho wanafanya wenzake kabla ya kuanza programu zake za mazoezi.

Baada ya kukaa kwa takribani dakika 20, Muangola huyo aliungana na baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao hawakuwa katika programu ya mazoezi ya nguvu na kuanza kuzunguka nao uwanja.

Baadhi ya wachezaji  ambao walikuwa wakifanya mazoezi hayo mepesi ni pamoja na , Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Yassin Mustapher, Kibwana Shomari, Wazir Junior, Abdallah Shaibu 'Ninja'.

Yanga walianza kwa kupasha misuli joto kisha wakagawanywa katika makundi mawili, moja likiwa na nyota kadhaa akiwemo Michael Sarpong, Haruna Niyonzima, Bakari Mwamnyeto, Farid Mussa na wengineo.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz