Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cannavaro wala hana presha Stars

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MENEJA wa Taifa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro' wala hana presha yoyote kuelekea mchezo wao wa marudiano wa kuwania Fainali za Chan 2021 akiamini suluhu waliyopata nyumbani dhidi ya Wakenya itawabeba ugenini.

Hata hivyo beki huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars amesema umakini wa wachezaji kwenye mchezo huo wa ugenini uakaopigwa Jumapili hii ndio utakaowabeba na kusonga mbele.

Cannavaro amesema kama vijana watakwenda kupambana na wakaweza wakatoka sare hata ya bao 1-1 basi itakuwa nafasi kwao kusonga mbele kwa kupata bao la ugenini.

Amesema wanaendelea kuzungumza na wachezaji kuona fursa iliopo kwenye suluhu hiyo na kudai kama wataitumia vyema basi wataibuka mashujaa kwa kitu ambacho kimekatiwa tamaa na Watanzania wengi.

"Ujue shujaa ni yule mtu anayefanya kitu cha kitofauti kwa mtu ambao  haujatarajiwa, Watanzania walitegemea Stars wangepata matokeo nyumbani, ila kwa kuwa ni suluhu sisi tukapambane kusaka bao la ugenini kitu anachoamini kitawapa moyo," amesema na kuongeza;

"Kwanza wao ndio watakuwa na presha ya mchezo hivyo sisi tukatumia hilo kucheza kwa utulivu na kuwaonyesha kwamba tunaweza kufanya maajabu tofauti na namna ambavyo watatuchukuliwa kwa wepesi."

Licha ya Cannavaro kujipa moyo huo, lakini Stars inapaswa kujiandaa kutokana na rekodi za ushiriki wa michuano hiyo iliyoasisiwa mwaka 2008 na Tanzania kushiriki fainali moja tu ya 2009, kuiangusha timu hiyo.

Katika michuano ya kati ya mwaka 2011-2018, rekodi zinaonyesha Stars haijawahi kupata matokeo mazuri ugenini katika mechi za kuwania ushiriki wa fainali hizo, kitu ambacho ili kuvunja mwiko huo ni lazima iendea kwa tahadhari na kupata mabao mapema.

xxxxxxxxxxxx

Chanzo: mwananchi.co.tz