Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Canelo amuomba msamaha Lionel Messi

Goal   Web Two Way Split  0557ef31 8420 4290 B50e A243503518e0 Canelo amuomba msamaha Lionel Messi

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Saul Canelo Alvarez amemuomba msamaha Lionel Messi baada ya kumshutumu mshambuliaji huyo wa Argentina kwa kutoheshimu bendera ya Mexico katika Kombe la Dunia.

Nyota huyo wa ndondi alijibu kwa hasira baada ya video kutoka kwenye chumba cha kubadilishia nguo kufuatia ushindi wa 2-0 wa Argentina dhidi ya Mexico ikimuonyesha Messi akishika shati ya Mexico kwa mguu wake wakati wa sherehe, iliyokuwa sakafuni.

Canelo alitangaza “Namwomba Mungu nisimpate” lakini, baada ya kukosolewa na watu wengi kuokana na kauli yake, sasa amerudi nyuma na kuomba msamaha kwa nahodha huyo wa Argentina.

“Siku hizi chache zilizopita nilibebwa na mapenzi na mapenzi ninayohisi kwa nchi yangu yakafanya nitoe maoni ambayo hayakuwa sawa na ninataka kumuomba msamaha Messi na watu wa Argentina,”

Canelo aliandika kwenye Twitter kuwa; “Kila siku tunajifunza kitu kipya na wakati huu ilikuwa zamu yangu, nazitakia timu zote mbili mafanikio katika mechi zao na hapa tutaendelea kuisaidia Mexico hadi mwisho”

Pande zote mbili zilitinga katika hatua ya mwisho ya mechi za Kundi C zikiwa na matumaini ya kutinga hatua ya mtoano ya michuano hiyo, huku Argentina ikifuzu hatua ya 16 bora baada ya kuitwanga Poland,wakati Mexico ikiitwanga Saudi Arabia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live