Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cambiasso wafunguka

Cambiaso Pic Data Cambiasso wafunguka

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MKURUGENZI mkuu wa kituo cha Cambiasso Sports Academy, Zuberi Kambi ameamua kuweka wazi tetesi zinazoenea kuhusu kuwachukua wachezaji wa kituo cha Moro Kids bila kuwasiliana na Uongozi wa kituo hiko.

Tetesi hizo zilianza kusambaa hivi karibuni kupitia kituo kimoja cha redio nchini na baadaye kupotea huku ikielezwa kwamba walishaweka suala hilo sawa.

Mwanaspoti lilimtafuta Kambi na alisema tetesi hizo kweli zilikuwepo lakini kulikuwa na sintofahamu ya uelewa katika masuala  ya soka la Vijana.

"Unajua mtoto wa chini ya miaka 17 hawezi kusainishwa mkataba, kwahiyo nilishangaa kusikia hivyo vitu kwani natambua utaratibu ulivyo".

Kambi alisema namna alivyokutana na wachezaji hao ilikuwa walipokuwa katika kambi ya timu ya Taifa kwa vijana chini ya miaka 20 iliyoenda Morocco na baadaye mashindano yalihairishwa.

"Tulienda pale na tukaongea nao vijana na kwa yule ambaye alikuwa na kituo basi tuliwasiliana na watu wao, wale ambao wanasimamiwa na wazazi tuliongea na wazazi wao pia".

Aliongeza kwa kusema upande wa Moro Kids walishaweka sawa jambo lao na kwasasa wanashirikiana kwa pamoja na kama kutakuwa na mchezaji mzuri basi anaenda katika Akademi yake.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz