Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Caicedo: Msimu wa kwanza Chelsea ulikuwa mgumu

Moises Caicedo Aeleza Kwa Nini Alichagua Kuhamia Chelsea.png Moises Caicedo

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Chelsea Moises Caicedo amesema msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo ulikuwa mgumu na alipoteza kujiamini kwa sababu ya shinikizo la bei yake ya pauni milioni 115.

Mchezaji huyo wa Ecuador mwenye umri wa miaka 22 alijiunga na The Blues kutoka Brighton Agosti, 2023 kwa ada ya pauni milioni 100 ambayo ingeongezeka hadi pauni milioni 115 kufuatia vita ya zabuni iliyohusisha Liverpool.

Alifunga bao moja na kutoa pasi nne za mabao katika mechi 48 katika msimu wake wa kwanza huku Chelsea ikimaliza nafasi ya sita Ligi Kuu England(EPL) na kocha Mauricio Pochettino akiondoka mwezi Mei.

"Mwanzo ulikuwa mgumu kwangu, kwa sababu uko kwenye klabu kubwa, bei, unapaswa kushinda kila mechi. Lakini baada ya miezi minne au mitano ya mwisho, nilihisi furaha zaidi katika klabu," amesema Caicedo.

Kocha mpya Enzo Maresca ameanza kazi Chelsea, na hivi ndivyo Caicedo alivyosema kuhusu kocha huyo wa zamani wa Leicester City boss: "Anafundisha mfumo ule ule niliocheza Brighton."

Liverpool ilikubaliana na Brighton dili la pauni milioni 111 kumsajili Caicedo kabla hajachagua kujiunga na Chelsea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live