Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cafu aponda Wabrazil wanaokimbilia Ligi Kuu ya Uingereza

Caf377556 Cafu aponda Wabrazil wanaokimbilia Ligi Kuu ya Uingereza

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa zamani wa Brazil, Marcos Evangelista de Morais maarufu kama Cafu amesema kutokana na wachezaji wengi qa Taifa hilo kukimbilia kucheza Ligi Kuu ya Uingereza, anaiona nafasi ya timu yao ya Taifa kupata ubingwa wa Kombe la Dunia ni ndogo.

Caf (53) ambaye ni beki wa kulia amewahi kuzichezea Real Zaragoza, AS Roma na AC Millan amewahi kutwaa ubingwa wa kombe la Dunia akiwa na Timu yake ya Taifa ya Brazil mwaka 1994 na mwaka 2002 huku akicheza pia fainali ya mwaka 1998 ambapo bingwa alikuwa Ufaransa.

"Nina hofu, kadri tunavyozidi kuwa na Wabrazil wanaohamia Ligi Kuu England ndivyo nafasi ndogo kwa Brazil kutwaa Kombe la Dunia inaongezeka.

"Hebu fikiria kuwa kila wiki unatolewa akili na vyombo vya habari kwamba wewe ni bora zaidi duniani, wakati huo huo si karibu bora.

"Napendelea La Liga, kwa sababu wana mawazo ya juu ya kufika fainali na kushinda. Katika La Liga hawana mdomo mbele ya kamera za TV wanaosema uwongo kuhusu wachezaji wa Uhispania au kuwadanganya ulimwengu. Wanazungumza mpira wa miguu huko, sio hadithi.

"Niliwasikia wakisema kuwa beki wa kulia wa Liverpool yuko kwenye kiwango changu kwenye nafasi hiyo ya beki wa kulia. Sikutaka kujadili, kwa sababu nilijua Vinicius atauonyesha Ulimwengu ukweli na alifanya huko Paris," amesema Cafu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live