Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cadena atema cheche Simba

Dani Cadena 13.jpeg Cadena atema cheche Simba

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unyama Unarudi. Ndiyo kauli waliyokubaliana viongozi na wanachama wa Simba kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Jumatatu jijini Dar es Salaam, kilichojadili mambo mengi yanayoihusu timu hiyo lakini kubwa zaidi ikiwa ni kurejesha makali, ubora na ubabe wa timu hiyo kwenye soka la Afrika.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, pamoja na mengi yaliyojadiliwa ilikuwemo pia namna ya kuanza kibabe hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kwenye mchezo wa Jumamosi hii, dhidi ya Asec Mimosas kutoka Ivory Coast.

Simba imepanga kuanza kwa ushindi mkubwa kwenye mechi hiyo, na moja kwa moja wanachama waliohudhuria kikao hicho waliwaagiza viongozi kuwafikishia ujumbe wachezaji na benchi la ufundi kuwa wamechoka kutambiwa mtaani na sasa wanataka kila mchezaji ajitume kadri awezavyo ili kurejesha heshima yao pia wakisisitiza hawatamvumilia mchezaji atakayezingua.

“Kila Mwanachama wetu anaitakia heri Simba, mambo mengi chanya yalijadiliwa na tunayafanyia kazi, lengo ikiwa ni kurejesha na kurinda ufalme wetu kwenye soka la Afrika,” alisema Imani Kajula Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba.

CADENA ATEMA CHECHE

Licha ya viongozi wa Simba kujadili kwa kina jina la kocha Mtunisia Radhi Jaidi lakini bado hawajafika mwafaka na kua asilimia kubwa za kocha mpya ni kupatikana kabla ya mechi na Asec Mimosas ili akae jukwaani kwanza kama shabiki taratibu zikiendelea.

Cadena na Matola wamepewa majukumu yote ya kuandaa timu kwaajili ya mechi na Asec, Mhispaniola huyo ana leseni ya UEFA Pro, na Seleman Matola ambaye ni mzoefu wa soka la Afrika akilitumikia kwa miaka mingi kama mchezaji na baadae kocha.

Akizungumza na Mwanaspoti, Cadena amesema maandalizi kambini yanaendelea vizuri na wanatengeneza timu itakayoshinda mechi zijazo huku ikicheza soka safi.

“Kwa sasa tunafayia kazi mechi ijayo na Asec. Tumeingalia timu hiyo, inacheza vizuri hivyo tumejipanga kuidhibiti lakini lengo kuu ikiwa ni kupata ushindi nyumbani,” alisema Cadena na kuongeza;

“Simba inarekodi nzuri kwenye michuano hii hususani inapokuwa nyumbani, hatutaki kupoteza rekodi hiyo bali kuiendeleza na kumfanya kila mpinzani atambue uhatari wa Simba.”

ASEC WATUA DAR

Wakati Simba ikiendelea kujifua, Asec Mimosas wametua nchini leo tayari kwa maandalizi ya mwisho wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa 3-1 na Simba katika uwanja wa Mkapa, Februari 13, 2022 hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa licha ya kwamba walilipa matokeo hayo kwenye mechi ya marudiano wakishinda 3-0, nyumbani Machi 20, 2022. Timu zote zitaingia kwenye mechi hiyo zikiwa zimevalia jezi mpya zilizoandaliwa maalumu kwa mashindano hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live