Manchester United inataraji kushuka dimbani saa 5:00 Usiku wa Leo Jumatano 23, 2022 kucheza dhidi ya Atletico Madrid ya Uhispania kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano hatua ya 16 bora Michuano ya klabu bingwa Barani Ulaya.
Kuelekea kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye dimba la nyumbani la Atletico Madrid 'Wanda Metropolitano', Atletico huenda wakamkosa kiungo wake nahodha Koke anayesumbuliwa na maumivu ya misuli.
Kwa Upande wa Manchester United, wao wanataraji kumkosa mshambuliaji wake Edinson Cavani kutokana na majeraha ya mguu yanayo sumbua mara kwa mara hususani msimu huu.
Gumzo linabaki kwa nyota wa zamani wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo 'CR7' ambaye anarekodi bora sana mbele ya Atletico Madrid kwa kufunga magoli 25 na kutoa assist 9 dhidi ya watukutu hao wa Diego Simeone.
Imani kubwa ya mashabiki wa Manchester United ipo kwa mkali huyo wa kufumania nyavu ili kuubeba mchezo huo kutokana na rekodi hiyo ambapo mara ya mwisho kuifunga Atletico ilikuwa mwaka 2019 kwenye michuano hiyo akiwa Juventus.
Mchezo mwingine wa hatua ya 16 bora ni ule utakaowakutanisha Benfica dhidi ya Ajax ya Uholanzi ambapo mshambuliaji wa Ajax, Sebastien Haller ambayo anaongoza kwa ufungaji msimu huu, magoli 10.