Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CR Belouzidad walicheza na akili za Yanga

CR Belzouidad Matokeo.jpeg CR Belouzidad walicheza na akili za Yanga

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga juzi walipoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya CR Belouzidad.

Mwenyeji hakupata matokeo tu kwa bahati mbaya bali ilikuwa ni mipango ambayo Mwalimu aliifanyia mazoezi.

CR Belouzidad wameudhibiti vema mchezo bila ya mpira. Na wamehakikisha nafasi chache walizozichagua zinahesabu.

Yanga wameutawala mpira lakini wapinzani waliwazuia kuutawala kwenye maeneo hatari kitu ambacho kilikuwa kinawalazimu kwanza wawe kwenye presha ya kufanya majaribio pindi tu wakiona uwazi kwani walinyimwa utulivu wa kuonana kama ambavyo wangetaka lakini pili wamejikuta wakiingia kwenye mtego wa kupeleka watu wengi mbele na ndipo wapinzani wakazihesabu pasi zao mpaka langoni kwao na kuwaumiza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: