Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CR Belouizdad watua Dar kibabe kuikabili Yanga

Cr Belouizdad Dar CR Belouizdad watua Dar kibabe kuikabili Yanga

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Timu yya Soka ya CR Belouizdad ya nchini Algeria imetua nchini Tanzania leo Jumatano, Februari 21, 2024 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga.

CR Belouizdad wametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, majira ya saa 10 jioni wakiwa na ndege binafsi, tayari kuwakabili Wananchi wa Mitaa ya Jangwani.

Ujio huo wa mapema wa CR Belouizdad ni kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ya Dar kabla ya mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Februari 24, 2024 majira ya saa 1:00 jioni katika Dimba la Mkapa.

Jotoridi la Dar es Salaam kwa siku za usoni linazoma nyuzijoto sentigredi za Celsius 27 hadi 33, wakati huo hali ya unyevu ni asilimia 80 hadi asilimia 90.



Boubou Traore raia wa Mali ndiye atakuwa mwamuzi huku mwamuzi mmoja pekee wa Burkina Faso (kwa kina Aziz Ki) akiteuliwa pia kuwa msaidizi na waamuzi wengine wote sambamba na viongozi wa mchezo huo watatoka Mali, nyumbani kwao Djigui Diarra.

Yanga wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya CR kwa bao 3-0 nchini Algeria mwishoni mwa mwaka jana.



Lakini pia ifahamike kuwa, Al Ahly ndiye anaongoza kundi lao kwa alama 6, CR Belouizdad nafasi ya pili na alama 5, Yanga wa tatu na alama 5 huku Medeama ya Ghana wakivuta mkia na alama nne, hivyo kimahesabu yeyote anaweza kufuzu kwenda hatua ya robo fainali iwapo atachanga vizuri karata zake kwenye michezo miwili iliyosalia.

Yanga SC wanahitaji halama tatu (3) muhimu kwenye mchezo huu kuweka kwenye hatua nzuri ya kuweka rekodi ya kufuzu hatua ya Robo Fainali ambayo mara ya mwisho tulifanya hivyo mwaka 1970.

Yanga SC wanashikilia nafasi ya tatu tukiwa na alama 5 kwenye kundi nyuma ya Al Ahly mwenye alama 6, Belouzidad akiwa na alama 5.



Yanga SC inashikilia rekodi pekee ya kuwa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kufuzu hatua ya Robo Fainali ambapo ilifanya hivyo mwaka 1969 & 1970 na kuwa klabu pekee ambayo imefunzu mara mbili mfululizo katika hatua hiyo kwa vilabu kutoka Tanzania.

Mwanzoni mwa msimu Rais wa Klabu ya Young Africans Eng Heris Said alisisitiza kuwa Klabu ina malengo na matarajio makubwa katika michuano ya kimataifa ili kuwa na mwendelezo wa kile kilichofanyika msimu uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live