Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CR Belouizdad waiwahi Yanga mapema tu!

Cr Belouizdad Celebrate CR Belouizdad waiwahi Yanga mapema tu!

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imesema kuwa, wapinzani wao kwenye mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, CR Belouizdad kutoka nchini Algeria wanatarajia kuwasili nchini keshokutwa, Jumatano, Februari 21, 2024 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo na Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe wakati akitangaza uzinduzi wa hamasa kuelekea mchezo huo wa marejeano utakaopigwa Jumamosi ijayo Februari 24, 2024 katika Dimba la Mkapa na kuupa mchezo huo jina la 'Pacome Day Kitaalam Zaidi'.

"Kwa taarifa ambazo tumewasiliana na CAF, Belouizdad wanatarajia kuingia nchini Jumatano saa 3:00 asubuhi asubuhi, kama kutakuwa na mabadiliko juu ya taarifa hii tutawajuza kadri ambavyo tutapata kutoka kwao," amesema Kamwe.

Katika mchezo wa kwanza timu hizi zilipokutana kule Algeria, Yanga ilikubali kuchezea kichapo cha bao 3-0, hivyo Wananchi wana kiu ya kulipa kisasi na kujitengenezea mazingira mazuri ya kwenda hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Ikiwa imesalia michezo miwili kukamilisha ratiba ya makundi, mpaka sasa Al Ahly anaongoa kundi akiwa na alama sita, Belouizdad nafasi ya pili na alama tano, Yanga nafasi ya tatu alama tano na Medeama anashika mkia akiwa nafasi ya nne na alama nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live