Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CR Belouizdad vs Al Ahly hakuna mbabe, kazi ngumu kwa Yanga

Ahly Cr Belouizdad CR Belouizdad vs Al Ahly

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi ya kiporo cha CR Belouzdad na Al Ahly katika Klabu Bingwa Afrika imeisha kwa sare na sasa Yanga wanashuka mpaka nafasi ya tatu kutoka nafasi ya pili.

Katika mchezo huo, CR Belouizdad wametengeneza nafasi 5 isivyo bahati kwao Goal keeper wa Al Ahly alikuwa bora. Al Ahly hawajatengeneza nafasi wala kupiga shuti lililolenga langoni. Ahly wamezidiwa kila eneo la uwanja huku wakiwakosa nyota wao (5) wa kikosi cha kwanza kama Tau, Dieng.

"Mechi ya mwisho ya hili kundi letu itakuwa kama mechi ya Fainali ya klabu bingwa Afrika na tutajaribu kufuzu kwa ushindi mzuri kama tulivyozoea" amesema Marcel Koller, Kocha Mkuu wa klabu ya Al Ahly akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika.

CR Belouizdad vs Al Ahly, hii mechi inatosha kuwapa dira Yanga jinsi ya kukabiriana na mpinzani wake Februari 24.

Yanga SC inahitaji alama nne (4) iweke rekodi nyingine ya kwenda robo fainali ya CAFCL, ishinde mchezo dhidi ya CR Belouizdad nyumbani na ikatafute sare ugenini kwa Al Ahly itafikisha alama tisa (9) kwenye Kundi, CR Belouizdad ikishinda na Medeama itafikisha alama nane (8).

MSIMAMO WA KUNDI D

Chanzo: www.tanzaniaweb.live