Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CR Belouizdad ni kipimo sahihi cha gamondi leo

Gamondi Coastal CR Belouizdad ni kipimo sahihi cha gamondi leo

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amesema kuwa mechi dhidi ya CR Belouizdad itakuwa kipimo sahihi kwa Kocha Mkuu wa Yanga, Angel Miguel Gamondi.

Yanga wanatarajia kuingia dimbani leo kumenyana na Belouizdad ikiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga wakiwa na kumbukumbu ya kutoshiriki michuano hiyo kwa miaka 25.

"Inawezekana hii mechi ikawa ndio ikawa kipimo sahihi cha ubora wa mbinu za kocha Miguel Gamondi, kwa sababu tangu msimu huu uanze mechi kubwa ambazo Yanga amecheza amekuwa akiingia kama favorite.

"Angalia mechi na Al Merrick, mechi na Azam (Ngao ya Jamii na Ligi), mechi na Singida, mechi na Simba (Ngao ya Jamii na Ligi), zote yanga aliingia kama favorite, lakini yawezekana mechi ya kesho (leo) Yanga ndio mechi pekee msimu huu akaingia akiwa sio favorite wa mchezo.

"Kwa hiyo tukianza kwenye game approach ya Miguel Gamondi na selection ya kikosi kuelekea siku ya kesho na namna timu ambavyo itacheza kwangu mimi ndio itakuwa siku ya kwanza ambapo naenda kuupima ubora wa Miguel Gamondi," amesema Wakanda Republic.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: