Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

COVID-19 yaigaragaza Chelsea

Chelsea Covid Chelsea inapitia wakati mgumu kutokana na wachezaji wake kuugua COVID-19

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Thomas Tuchel anasema kuwa wanalazimika kuanza upya tena, baada ya kupanga kikosi na wachezaji kupatikana na maambuzi ya Covid.

Tuchel sasa anapanga kuingiza wachezaji wengi wa Akademi dhidi ya Brentford kwenye Carabao Cup, na bosi anakiri kuwa hii imekuwa changamoto kwa Chelsea.

Baadhi ya wachezaji ambao tayari walikuwa kwenye mpango wa Tuchel, akiwepo Lewis Baker wamepatikana na maambukizi ya Covid, na Tuchel amelazimika kuwa na mpango mbadala.

Changamoto kubwa kwa Tuchel ni kuwa hata anavyoweka mipango ya mazoezi anakuwa hana uhakika na wachezaji wangapi wanawasili.

N’Golo Kant, Trevoh Chalobah na Andreas Christensen wanapambania majeraha yao. Huku Jorginho akiwa anarejea dimbani baada ya kupatikana bila maambukizi.

Lakini, Kai Havertz, Ruben Loftus-Cheek, Romelu Lukaku, Timo Werner, Callum Hudson-Odoi na Ben Chilwell wote watakuwa wanakosa mchezo wa wikiendi hii kwa mara nyingine.

“Hii ndiyo hali. Kuwa na wachezaji 13 au 14 kwa mechi moja, ni tatizo. Lakini sio tatizo kubwa sana tutapambana kwa kila hali, ndivyo tutafanya kesho.” – Thomas Tuchel

Chanzo: www.tanzaniaweb.live