Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CEO wa Yanga anaipaka matope klabu

Okrah Mtineeeeee CEO wa Yanga anaipaka matope klabu

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CEO wa Klabu ya Yanga SC, Andre Mtine anaipaka matope klabu hiyo. Sikumbuki hii ni mara ya ngapi Yanga SC inafungiwa kusajili ndani ya mwaka huu, nadhani ni mara ya (3).

Klabu kubwa kama Yanga kila mara kuwa kwenye headlines za kufungiwa kusajili tena kwa kushindwa kulipa wachezaji pesa ndogo kabisa zilizo ndani ya uwezo wao inatafsirika kuwa klabu hiyo ina kiburi.

Madeni na vitu kama hivyo ni jukumu la CEO kuhakikisha yanalipwa. Mtine kafanya mambo mengi sana mazuri lakini vitu vidogo kama hivi vinachafua jina lake na jina la Taasisi kwa ujumla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live