Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CEO Yanga: Hatuna hofu na Mamelodi

Andre Mtine.jpeg Andrew Mtine.

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtendaji Mkuu wa Yanga SC, Andrew Mtine amesema kikosi chake hakina hofu na Mamelodi Sundowns katika mchezo wao wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo utapigwa katika Dimba la Mkapa, Jumamosi Machi 30, 2024 kuanzia saa 3:00 usiku.

"Lazima tuwe na imani kwamba tunaweza kuwashinda na kusonga mbele. Na kutambua hilo, wachezaji wanapaswa kutoa 100% kwa ajili ya timu."

"Mashabiki lazima washangilie timu na kutupa sapoti inayohitajika. Tunaiheshimu Sundowns kwa sababu ni timu kubwa na yenye mafanikio, lakini hatuna hofu nao. Utakuwa mchezo mkubwa na tuko tayari kwa lolote."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: