Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CEO Mtibwa Sugar afurushwa

Swabri Aboubakar (22).jpeg Swabri Aboubakar.

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtibwa Sugar inadaiwa kuachana rasmi na aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Swabri Aboubakar ikiwa ni miezi miwili tu tangu gazeti hili kuripoti taarifa za kuachwa kutokana na kile alichoambiwa kujitafakari katika nafasi yake.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo zinadai, Swabri ameshapewa mkono wa kwaheri na viongozi na tayari wameanza mchakato wa kutafuta mbadala wake ambaye ataweza kuiziba vyema nafasi hiyo ndani ya kikosi hicho.

“Ni kweli ameondoka hapa kwa kuwa timu inafanya vibaya kwa msimu wa pili mfululizo, tunahitaji kujinasua hapa tulipo hivyo tumeona tufanye marekebisho kwa mustakabali wa klabu,” kilisema chanzo chetu.

Kwa upande wa Ofisa Habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru alipotafutwa na Mwanaspoti kuzungumzia jambo hilo alisema kwa sasa hawezi kuzungumza hilo kwani wamekuwa na vikao mbalimbali kwa ajili ya kujadili mambo kadha wa kadha yanayowahusu.

“Tuna vikao kwa sasa vinavyoendelea tukijadili mambo mbalimbali ikiwemo suala la usajili ambalo ndio kubwa zaidi kwa sababu sehemu tuliyopo kwenye msimamo sio salama kwetu hivyo ni lazima tuandae mipango mizuri ili kujinasua,” alisema.

Hata hivyo, Mwanaspoti linatambua Swabri tayari ameanza kutafutiwa mbadala wake na muda wowote kuanzia sasa atatangazwa rasmi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live