Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CEO Kagera Sugar apewa cheo Yanga

Ibrahim Mohamed Kagera Aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (Ceo) wa Kagera Sugar, Ibrahim Mohamed

Sat, 20 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (Ceo) wa Kagera Sugar, Ibrahim Mohamed anatajwa kutua Jangwani, akitarajiwa kutambulishwa kama Mkurugenzi wa Idara ya Mashindano.

Kigogo huyo alikuwa katika msafara wa Yanga ulioondoka juzi jijini Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kambi ya siku 16 itakayoenda na michezo mitatu ya kirafiki ya kimataifa ukiwamo wa leo jioni dhidi ya Fc Augsburg ya Ujerumani, huku taarifa zikisema tayari ameanza kazi kimya kimya.

Mohammed ametua Yanga akitarajiwa kutambulishwa kama Mkurugenzi mpya wa Idara ya Mashindano ya timu hiyo, klabu hiyo ikivutiwa na uzoefu wake.

Ingawa, Yanga bado hawajatoa taarifa rasmi lakini tayari Mohammed yuko na timu hiyo Afrika Kusini na kikosi cha timu hiyo.

Mohammed anatua Yanga akitokea Kagera Sugar alipokuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, ambapo aliondoka baada ya mkataba wake kumalizika mara baada ya msimu wa Ligi Kuu uliopita kumalizika.

Kigogo huyo pia amewahi kufanya kazi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akiwa katika Idara ya Mashindano kabla ya kutimkia Kagera Sugar.

Mohammed anakuwa kigogo wa pili kuchukuliwa na Yanga ambapo mapema mabingwa hao walimchukua Walter Harrison aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa KMC na kwenda kuwa meneja wa timu hiyo.

Yanga imeweka kambi ya muda mjini Mpumalanga na leo itacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu ya Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), Augsburg kabkla ya Julai 24 kumenyana na wenyeji wao TS Galaxy ya huko Sauzi na kumaliza kambi kwa kucheza na Kaizer Chiefs katika mechi ya Kombe la Toyota, siku ya Julai 28 na siku mbili baadae itarejea nchini kwa Tamasha la Wiki ya Mwananchi Agosti 3 kisha kucheza mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba siku ya Nane Nane ikipigwa Kwa Mkapa.

Chanzo: Mwanaspoti