Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#CAFCLDraw: Yanga SC yapangiwa AS Ali Sabieh ya Djibouti

Yanga Squad Full Kikosi cha Yanga.

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania, Klabu ya Yanga kwenye hatua ya awali mtoano ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CL) imepangwa kucheza na timu ya 2023/24 Association Sportive d'Ali Sabieh( ASAS) ya Djibouti.

Michezo ya raundi ya kwanza itapigwa kati ya Agosti 18, 19 na 20, mwaka 2023 na marudiano yatakuwa Agosti 25, 26 na 27 wakati raundi ya pili itachezwa Septemba 15, 16 na 17 na marudiano yatakuwa Agosti 29, 30 na Oktoba 1, 2023.

Aidha katika michezo hiyo, raundi ya kwanza Yanga ataanzia ugenini na endapo atafanikiwa kutinga raundi ya pili pia ataanzia ugenini.

Msimu uliopita Yanga walibeba ubingwa wa Tanzania na Ubingwa Shirikisho huku wakifanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika hatua za awali za Kombe la Mabingwa na kutupwa Shirkisho.

ASAS ndiyo mabingwa mara nyingi zaidi wa Djibouti wakiwa wamebeba ubingwa huo mara (7). ASAS wana nyota wa kimataifa 5 ikiwemo 3 kutoka Burundi.

Endapo itavuka hatua hii itakutana na mshindi kati ya El Merrick ya Sudan ama Association Sportive Otohô ya Congo Brazaville ambao ni mabingwa wa nchi hiyo.

Al Merreikh wao msimu uliopita walifanikiwa kutinga hatua ya Makundi ya Kombe la Mabingwa Afrika kwa bao la ugenini baada ya kutoka jumla ya bao 3-3 na Al Ahly Tripoli ya Libya.

Katika hatua ya Makundi, katika michezo 6, Al Merreikh ilimaliza mkiani ikiwa na alama 5, ikishinda mechi moja, sare 2, kupoteza 3, mabao ya kufunga 5 na mabao ya kufungwa 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live