Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#CAFCL: Yanga yapangwa na A Ahly, rekodi zinasemaje?

Yanga Gamondi Wachezaji Yanga yapangwa na A Ahly CAFCL

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika Droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezeshwa leo Oktoba 6, 2023 na Shirikisho la Mpira Afrika (CAF), Klabu ya Yanga kutoka Tanzania imepangwa kundi D pamoja na bingwa mtetezi wa Kombe hilo Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad ya Algeria anayoichezea Simon Msuva na Medeama SC ya Ghana.

Mechi za raundi ya kwanza zitapigwa Novemba 24 na 25, raundi ya pili Desemba 1 na 2, raundi ya tatu ni Desemba 8 na 9, raundi ya nne ni Desemba 19, raundi ya tano ni Febdruari 23 na 24 na raundi ya sita na ya mwisho ni Machi 1 na 2 kisha zitapangwa Robo Fainali mpaka Fainali.

Mara ya mwisho Yanga kukutana na Al Ahly ilikuwa ni mwaka 2016 katika hatua ya pili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa ambapo Yanga ilitoa sare ya bao 1-1 nyumbani kisha ikaondolewa kwa kufungwa bao 2-1 ugenini, bao la Yanga likifungwa na Donald Ngoma.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2014, Yanga iliwahi kuifunga bao 1-0 kwenye michuano ya CAF Champions League. Yanga pia imewahi kupokea kipigo cha bao 5-0 kutoka kwa Ahly mwaka 1982.

Katika mechi 10 za mwisho walizokutana, Yanga imeshinda mechi moja, imeota sare 3 na kupoteza michezo 6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live