Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#CAFCL: Wananchi watakata kwa Mkapa, waipiga Medeama 3-0

Mudathir Pacomeee Wananchi kutoka mkiani mpaka nafasi ya pili

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi, Young Africans SC wamepata ushindi wa kwanza na wa kihistoria katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kushinda kwa 3-0 dhidi ya vigogo wa Ghana, Medeama.

Matokeo ya mchezo huo ambao umeoigwa majira ya saa 10:00 katika Dimba la Mkapa, yamefufuabmatumani ya Wananchi kufukuzia kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambayo hawajashiriki kwa miaka 25 sasa.

Yanga walianza kwa kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya CR Belouizdad ya nchini Algeria kisha sare ya bao 1-1 dhidi ya vigogo wa Afrika, Al Ahly kabla ya kutoa sare nyingine na Medeama.

Ushindi wa leo unaifanya Yanga kupanda kutoka nafasi ya mwisho mpaka nafasi ya pili lwenye msimamo wa kundi lao wakilingana alama 5 sawa na Ahly lakini tofauti ya idadi ya mabao ya kufunga nakufungwa ndiyo imewaweka Yanga nafasi ya pili.

FT: YANGA SC 3-0 MEDEAMA

⚽ Pacome Zouzoua 33'

⚽ Bakari Mwamnyeto 61'

⚽ Mudathir Yahya 66'

❌ Sowah anakosa penati dakika ya 55'

Sowah anakula kadi nyekundu dakika ya 90'

MSIMAMO KUNDI D

1️⃣ AL AHLY (pointi 5)

2️⃣ YANGA SC (pointi 5)

3️⃣ CR BELOUIZDAD (pointi 4)

4️⃣ MEDEAMA (pointi 4)

Al Ahly na Belouizdad hawajacheza raundi ya nne ya hatua ya makundi kutokana na ushiriki wa Al Ahly kwenye michuano ya kombe la Dunia ngazi ya Klabu.

Kituo kinachofuata ni Yanga kuwakaribisha CR Belouizdad ambao kimahesabu ndio wapinzani wao wakuu wanaowania nao kupata nafasi ya kwenda robo fainali mbali na Ahly ambaye anaoekana yeye kufuzu hatua hiyo sio jambo kubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live