Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#CAFCL: Simba yapangwa na Wydad tena, rekodi zinasema hivi

Simba Wydad A0002 Simba yapangwa na Wydad tena CAFCL

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limepanga droo ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika Msimu wa 2023/2024. Tanzania ambayo inawakilishwa na Simba na Yanga Wawakilishi wao wamepangwa Kundi B na D.

Simba SC imepangwa Kundi B lenye Timu za Wydad Casablanca ya Morocco, Jwaneng Galaxy ya Afrika Kusini na Asec Mimosa ya Ivory Coast wakati Yanga imepangwa Kundi D na timu za Al Ahly ya Misri, Medeama ya Ghana na CR Belouizdad ya Algeria.

Ikumbukwe kuwa, msimu uliopita, Simba Sc walipangwa robo fainali ya michuano hiyo na Wydad ambapo Simba ilifanikiwa kushinda mchezo wa nyumbani kwa bao 1-0, kisha ikafungwa ugenini kwa bao 1-0 na Simba kuondolewa kwenye michuano hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Mnamo Mei 28, 2011 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Wydad Casablanca

iliifunga Simba SC bao 3 - 0, kisha Simba akatoa sare ya bila kufungana katika Dimba la Mkapa.

Mechi za raundi ya kwanza zitapigwa Novemba 24 na 25, raundi ya pili Desemba 1 na 2, raundi ya tatu ni Desemba 8 na 9, raundi ya nne ni Desemba 19, raundi ya tano ni Febdruari 23 na 24 na raundi ya sita na ya mwisho ni Machi 1 na 2 kisha zitapangwa Robo Fainali mpaka Fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live