Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAFCL: Mwaka 1998 Yanga ilimaliza mkiani bila ushindi wowote

Yanga Algeria Tiziiiiii CAFCL: Mwaka 1998 Yanga ilimaliza mkiani bila ushindi wowote

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nilichokiona kwenye mchezo wa kwanza wa Yanga hatua ya makundi, ni kwamba Yanga imekaribishwa rasmi kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kupita miaka 25 bila timu hiyo kufuzu hatua ya makundi.

Takribani miaka 25 ipite Yanga kucheza hatua hiyo hakuweza kushinda mchezo wowote kwenye kundi lake ambapo alikuwa na miamba kama ASEC Mimosas aliyemaliza na alama 13, Manning Rangers alikuwa na alama 10, Raja Casablanca alama 8, na Yanga aliyemaliza na alama 2.

Katika kundi hilo Yanga alipokea vipigo vizito kama cha 6-0 dhidi ya Raja Casablanca, akapokea 3-0 kutoka kwa ASEC, akapokea 4-0 kutoka kwa Manning Rangers lakini mechi ya marudiano alitoa sare ya 3-3 na Raja, 1-1 na Manning Rangers.

Ni Meridianbet pekee unaweza kubashiri mechi za Ligi ya Mabingwa zikiwa na odds kubwa, leo acheza Simba vs ASEC mgeni huyu amepewa odds kubwa ya ili ashinde.

Mechi ya jana imetoa picha ya aina ya kundi alilopo Yanga, Mwalimu Gamondi mpango kazi wake wa mechi haukuwa mzuri, kwanini iko hivi mechi nyingi za hatua hii hususani timu za Afrika unapokuwa ugenini lazima umuheshimu mpinzani usifunguke moja kwa moja, lakini Yanga wao walifunguka na hivyo kuruhusu kufungwa kwa counter attack.

Wachezaji wa CR Belouzdad waliumaliza mchezo kiakili tu, waliwaacha Yanga wamiliki mpira wao wakachagua kumiliki matokeo, na miwsho wa dakika 90, Yanga kaambulia umiliki wa mpira mkubwa matokeo zero.

Kuelekea mechi zijazo Yanga inatakiwa atumie vizuri uwanja wake wa nyumbani kuanzia mechi ya Desemba 2 dhidi ya Al ahly kwani mwarabu yule huenda akaja na hasira zote.

Al ahaly wao ni waumini wa kushambulia kwa counter attack wakiwa ugenini, hivyo full back za Yanga hazitakiwi kupanda zote kwenda kushambulia kwani wakifanya hivyo watakuwa wanatoa mwanya kwa Percy Tau na Hussein El Shahat kushambulia kupitia pembeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: