Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAFCL: Fei Toto uso kwa uso na Mayele?

Mayele Fei Toto Fei Toto uso kwa uso na Mayele?

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Droo ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika imekamilika ambapo Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo ya CAFCL wamebaini wapinzani wao.

Young Africans Sc itaanzia ugenini dhidi ya Vilal’O ya Burundi huku Wanalambalamba, Azam Fc wakianzia nyumbani dhidi ya APR Fc ya Rwanda.

Mshindi wa matokeo ya jumla kati ya Yanga Sc dhidi ya Vilal’O Fc atachuana na mshindi wa matokeo ya jumla kati ya SC Villa ya Uganda dhidi ya Commercial Bank ya Ethiopia kwenye raundi ya kwanza.

Aidha mshindi wa matokeo ya jumla kati ya Azam fc dhidi ya APR Fc ya Rwanda atakabiliana na mshindi kati ya JKU Fc ya Zanzibar dhidi ya Pyramids Fc ya Misri.

HATUA YA AWALI

Vital’O (Burundi) vs Young Africans SC

Azam FC vs APR Fc (Rwanda)

JKU FC vs Pyramids FC (Misri)

Sc Villa (Uganda) vs Commercial Bank (Ethiopia)

Mechi za mkondo wa kwanza wa hatua ya awali zitapigwa kati ya Agosti 16 - 18 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Agosti 22 - 25, 2024.

Mechi mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza zitapigwa kati ya Septemba 13-15, 2024 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Septemba 20-22, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live