Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#CAFCL: Al-Merreikh vs Yanga rasmi kupigwa Rwanda

Yanga Merreikh A0013 Al-Merreikh vs Yanga rasmi kupigwa Rwanda

Sat, 2 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo kati ya El Merreikh ya Sudan dhidi ya Yanga sasa rasmi utapigwa Uwanja wa Pele nchini Rwanda.

Awali El Merreikh ilikuwa na hesabu za kuuhamisha mchezo huo kuupeleka nchini Morocco lakini inaelezwa walishindwa kupata visa kwa wakati kuwahi muda wa kikanuni wa kubadilisha uwanja.

Yanga imethibitisha kwamba mchezo rao wa kwanza ugenini dhidi ya El Merreikh utapigwa Uwanja wa Pele nchini Rwanda ambao awali ulijulikana kama Uwanja wa Nyamirambo.

Uwanja huo ambao umefanyiwa ukarabati mkubwa hauna kumbukumbu nzuri kwa Yanga kwani mara ya mwisho walipogusa hapo walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Rayon Sport mwaka Agosti 29, 2018.

Matokeo hayo yaliwatupa Yanga nje na kuipa nafasi Rayon kutinga makundi ya Kombe la Shirikisho wakati huo ikifundishwa na kocha Roberto Oliveira 'Robertinho' ambaye sasa yuko Simba.

Wasudan hao awali walitumia Uwanja wa Huye nchini Rwanda katika mchezO wao wa mtoano wa avwali kama Uwanja wao wa nyumbani walipolazimishwa suluhu dhidi ya AS

Otoho ya Congo Brazzaville, na El Merreikh kufuzu kwa faida ya bao la ugenini kufuatia mchezo wa kwanza kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live